VIDEO: “Lupita Nyong’o Is PEOPLE’s World’s Most Beautiful” on YouTube


Filamu ya kwanza ya Hollywood
ilimpa Lupita Nyong’o tuzo ya
kwanza ya Oscar. Na sasa jarida la
People limemtaja Mkenya huyo kuwa
ndiye ‘mtu mrembo zaidi duniani’
kwa mwaka 2014.

image

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
uhariri wa jarida hilo, Jess Cagle
Nyong’o alikuwa chaguo sahihi
kukava issue ya jarida hilo la
kutimiza miaka 25. “She is fantastic.
There really was no contest this year.
The way she carries herself with such
grace and humility, it put her over the
top. I just love her,” alisema. Jarida
hilo liliwahusisha wasomaji wake
kutaja mtu anayestahili kuchukua
heshima hiyo mwaka huu na Lupita
kupendekezwa na wengi.
Na sasa mrembo huyo ameungana
na wanawake wengine waliowahi
kukava issue ya kutimiza mwaka
wakiwemo Julia Roberts, Michelle
Pfeiffer, Beyonce Knowles, Drew
Barrymore na Jennifer Lopez. Kwa
miaka 25, jarida la People limekuwa
likitoa heshima hiyo na ni wanaume
watatu tu waliowahi kupata ambao
ni Mel Gibson, Tom Cruise na
Leonardo DiCaprio (1996, 1997 na
1998). Mwaka jana alikuwa muigizaji
Gwyneth Paltrow.
Lupita Nyong’o Is PEOPLE’s World’s Most Beautiful: http://youtu.be/CVLpgOOBgG0