G7 yazidi kuibana zaidi Urusi


image

Askari wa Ukraine
Viongozi wa nchi Saba tajiri kwa viwanda duniani G7
wamekubaliana kuongeza vikwazo zaidi kwa Urusi
ambapo wamesema imezidi kuifanya Ukraine
isitawalike.
Ikulu ya White House ya Marekani imesema wataanza
kuweka vikwazo hivyo haraka iwezekanavyo kuanzia
siku ya jumatatu na wanatarajia kulenga biashara za
binafsi na ambazo zina uhusiano na Rais Vladimir Putin
wa Urusi.
Viongozi hao wa G7 wameelezea kuguswa kwa na jinsi
Urusi ilivyoshindwa kuacha kuwasaidia wanaoipinga
serikali.
Wametoa wito kwa Urusi kuacha mipango yake kijeshi
ya siri kwenye mpaka na Ukraine.
Kwa upande mwingine viongozi hao wa nchi saba tajiri
duniani wameisifu Ukraine kwa jinsi walivyojizuia kwa
kupanda na wapiganaji waasi.
Serikali ya Ukraine imesema inahofia kuwa Urusi ina
mipango ya kuivamia. Hata hivyo Urusi imesema nchi
za magharibi zina mipango ya kuteka kuitawala nchi
yao.

Advertisements