Godzilla: Bado nina imani na waongozaji wa video wa Tanzania


Rapper Godzilla aka Zizi amesema bado ana imani
kuwa waongozaji wa video wa Tanzania wanaweza
kufanya video nzuri kama wasanii wakijiandaa kwa
nzuri.

image

Amesema anatarajia kumtumia Nick Dizzo kama
muongozaji wa video yake wimbo wake mpya ‘You and
I’ aliomshirikisha Marco Chali ambaye ameutayarisha
pia kupitia MJ Records. “Nick Dizzo ndiye
tuliyempendekeza na Marco,” Zizi ameiambia Bongo5.
“Kwasababu amefanya video kama za akina Izzo B
zimeenda Channel O zinapigwa. Ni kumpa vifaa tu na
kukodisha vifaa vya hela nyingi. Bado naamini wabongo
wana nafasi nzuri kwasababu ukiangalia watu
wanaofanya video nje zinaenda lakini sio zote
zinafanikiwa kupita sehemu wanazotaka. Kwahiyo
inategemea na upepo wa mtu ameangukaje,”
ameongeza.
“Mimi naamini kwenye watu wa ndani sana, mimi
naamini watu wana vitu vingi. Kuna mambo tu Bongo
yanatukwamisha labda kwa system ama vitu fulani
lakini watu wana uwezo mkubwa sana Tanzania.”
source: bongo5