Papa wawili watangazwa watakatifu


image

Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani
Umati mkubwa wa watu wamekusanyika mjini Vatican
kushuhudia tukio la kihistoria ambapo viongozi wawili
wa zamani wa Kanisa Katoliki, Papa John Paul II na
Papa John XXIII wametangazwa watakatifu.
Ibada iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Papa Francis
na mtangulizi wake Papa Benedict XVI imeangaliwa na
karibu mahujaji milioni moja na wengine mamilioni ya
watu kupitia matangazo ya televisheni na redio.
Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe
hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa
nchi na serikali.
Hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa
kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.
Waandishi wa habari wanasema hatua hii inachukuliwa
kama njia ya kuziunganisha kambi mbili za wapenda
mageuzi na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika
Kanisa Katoliki.

Advertisements