SNOOP DOGG, SHAQ NA MAGIC JOHSON WACHUKIZWA NA KAULI YA KIBAGUZI ILIYOTOLEWA NA MMILIKI WA CLIPPERS


image

Mmiliki wa Clippers Donald Sterling akiwa na mpenzi
wake aliyekaa kushoto kwake
Mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya Los Angels
Clippers ‘Donald Sterling’ amejikuta akiambulia matusi
na kujishushia heshima yake kutoka kwa wamarekani
weusi baada ya kauli za kibaguzi alizokuwa akimtolea
mpenzi wake wakati wa mazungumzo kudakwa kwenye
kinasa sauti hali iliyopelekea mastaa wakubwa kama
vile Snoop Dogg, French Montanna, Kobe brayant, Shaq,
Lebron na mchezaji wa zamani wa timu ya lakers Magic
Johnson kukasirishwa na kuamua kumtolea uvivu.
Licha ya timu yake kujaa wahezaji wengi weusi
waliopata kutwaa mataji mbalimbali makubwa, taarifa
zinasema kwamba Sterling hakutaka kabisa mpenzi
wake apige picha na mtu mweusi ikiwemo na sharti la
kutomleta rafiki yake yeyote mweusi katika mechi za
Clippers.
”Ni aibu kwa Donald Sterling kuonyesha ubaguzi kwa
watu wenye asili ya afrika. Timu yake ina wachezaji
wengi weusi ambao wanafanya kazi ya kumletea
ubingwa na kuongeza idadi kubwa ya mashabiki.
alisema Maagic Johnson.
Mtandao wa TMZ uliweza kuwahoji baadhi ya wacheza
kikapu na wanamuzikii mashuhuri kama vile Lebron,
Shaq, Kobe, Snoop na Montana, kuhusiana na kauli
tata alizotoa Sterling….

Advertisements