ZAMBIA YAOMBOLEZA KIFO CHA MTANGAZAJI GWIJI WA SOKA ‘DENNIS LIWEWE’ KWA SIKU TATU


image

Marehemu Dennis Liwewe
Jamii ya wanamichezo hususani wapenzi wa mpira wa
miguu nchini Zambia inaomboleza kifo cha mtangazaji
gwiji wa soka mzee Dennis Liwewe ambaye aliwahi
kuwa mwandishi wa habari za michezo wa BBC idhaa
ya kiingereza katika kipindi cha Focus on Africa.
Serikali ya Zambia imetangaza siku tatu za
maombolezo huku bendera kupepea nusu mlingoti kwa
heshima ya nguli huyo wa utangazaji.
Utangazaji wa Liwewe ulikuwa ni wa mzuka na hamasa
kwa soka la Zambia, hali iliyompelekea asafiri zaidi ya
mara 96 katika nchi 42 akiwa na timu ya Taifa ya soka
ya Zambia ijulikanayo kama Chipolopolo .
Mzee Dennis Liwewe ambaye alifariki hapo juzi akiwa
na umri wa 78, alifanya kazi ya utangazaji wa soka kwa
zaidi ya miaka 50 kabla ya kustaafu mwaka 1993 kwa
ushauri wa madaktari kufuatia mshituko wa moyo
alioupata kufuatia ajali ya ndege iliyouwa wachezaji
wote wa timu ya soka ya taifa ya zambia Aprili 28
mwaka huo ambapo yeye alinusurika ajali hiyo baada
ya kuchelewa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea nchini
Senegal.
Utangazaji wake wenye hamasa na uzalendo mkubwa
ulimfanya atambulike na kuheshimiwa nchini zambia
ambapo alichukuliwa kama mmoja wa watu maarufu
wenye ushawishi mkubwa .

Advertisements