DON JAZZY AWAZAWADIA MKOKO WA NGUVU MAHARUSI TIWA SAVAGE NA TEE BILLZ


Mwanamuziki Tiwa savage wa Nigeria na mume wake
Tee Billz wamefanya sherehe ya ndoa yao jijini Dubai
iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya watu mashuhuri,
ndugu, jamaa na marafiki kutoka sehemu tofauti, huku
mwanamitindo daraja la kwanza kutoka Tanzania
asiyekuwa na chembe ya skendo ‘Millen Magese’
alikuwawa miongoni mwa wageni waalikwa.
kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Nigeria unaoandika
habari za mastaa ulisema ya kwamba Sherehe hiyo
ilifanyika kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano
‘Armani’ . Baadhi ya mastaa nyota wa nigeria waliopata
nafasi ya kuhudhuria ni pamoja na Bank W aliyekuwa
best man wa bwana harusi, Don Jazzy, Lola Omotayo-
Okoye, Toke makinwa, Dr Sid, Tolu Oniru, Eku Edewor,
Seyi Shay, Tania Omotayo na wengine wengi.
Mmiliki na mwanzilishi wa studio ya Mavin yenye
makazi yake Lagos, Nigeria Michael Collins Ajereh AKA
Don Jazzy alinogesha sherehe hiyo baada ya
kuwazawadia maharusi gari mpya aina ya Toyota Prado
ya rangi nyeusi hali iliyopelekea ukumbi kulipuka kwa
shangwe. Nisikuchoshe sana…Tazama Picha hapo chini
uone ilivyokuwa.

image

Tee Billz

image

Tiwa Savage
Source 360nobs

Advertisements