Huu ni wimbo uliowakutanisha wasanii 50 kutoka Tanzania unaohusu Muungano.


image

Wimbo Maalumu wa Muungano ulioimbwa na wasanii
50 kutoka Tanzania ambao kwa pamoja walikaa na
kutengeneza wimbo huu,jina la wimbo huu unaitwa
Tuulinde umetayarishwa na maproducer wawili Ema the
boy na Tuddy Thomas kutoka Soround Sound Studio.
Wimbo huu maalumu wa Muungano umeimbwa kutoka
katika mahadhi tofauti tofauti ya muziki wa hapa
Tanzania kuna wa Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop
na muziki wa injili.
Inawezekana ikawa mara ya kwanza katika historia ya
nchi yetu,wasanii 50 tofauti kuimba wimbo kwa
pamoja,kwa ushirikiano mkubwa,wasanii hawa
wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio
utanzania wetu.
Miongoni mwa wasanii ambao utazisikia sauti zao ni
pamoja na Kadjanito,Mwasiti,Linah,Christina
Shusho,Khadija Kopa,Frola Mbasha,Ommy
Dimpoz,Diamond,Josse Mara,Kalala Jr,Ali Kiba,Peter
Msechu,Mrisho Mpoto,Abdul Kiba,Mzee
Yusuph,Angel,Mwana Fa,Nikki Wa pili,G Nako,God
Zilla,Madee,Asley,Shaa,Mandojo,Domokaya,Shilole na
Roma Mkatoliki.
Bonyeza play kusikiliza wimbo huu

Advertisements