KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN WATALAZIMIKA KUFUNGA NDOA MARA TATU, MOJA MAREKANI NA MBILI UFARANSA


Zikiwa zimebaki siku chache kabla wazazi wa North
West hawajaungana na kuwa mwili mmoja,
imefahamika kuwa mastaa hao Kanye West na mama
wa mwanaye Kim Kardashian watalazimika kufunga
ndoa mara tatu.

image

Mtandao wa Radar Online umeripotia exclusive kuwa
ndoa ya wawili hao inatarajiwa kuwa na hatua mbili
kabla ya ile ya mwisho itakayofanyika Paris, Ufaransa
mwishoni mwa mwezi ujao.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani, ndoa ya kwanza ya
Kim na Kanye itafungwa Kusini mwa California huku ya
pili na ya tatu zitafungwa Ufaransa.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa mwanasheria wa
wachumba hao amewashauri waanze kwa kufunga
ndoa ya kiserikali wakiwa `Marekani, kabla ya ile kubwa
ya Ufaransa ya May 24 ili kuepukana na vikwazo vya
kisheria.
“Typically, the U.S. recognizes citizens getting married
in France, but dealing with a foreign government and
paperwork could be a nightmare,” Chanzo hicho
kilisema. “So just to make sure it’s legal, Kim and Kanye
will first be having a civil ceremony in Southern
California.”
Baada ya hapo ndipo wapenzi hao wataelekea Paris,
ambako nako sheria ya Ufaransa inahitaji wanandoa
kuwa na sherehe mbili za ndoa. Yaani Kabla ya ndoa ya
kanisani kufungwa cheti cha ndoa ya kiserikali
huhitajika.
“A religious ceremony has to be performed after a civil
ceremony, never before,” Ubalozi wa Ufaransa ulioko
Washington D.C ulliambia Radar Online.

Advertisements