NACTE YATOA UTARATIBU MPYA KUOMBA VYUO KWA 2015


image

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) limesema
kuanzia mwaka huu wa masomo, wanafunzi
wanaotaka kujiunga na masomo ngazi ya astashahada
na stashahada ya utabibu na ualimu, watatakiwa
kuomba katika mfumo wa pamoja wa mtandao wa
Central Admission System (CAS) na siyo vyuoni kama
ilivyozoeleka.
Katibu Mtendaji wa Nacte, Dk. Primus Nkwera, alitoa
taarifa hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya
maazimio mbalimbali ya kikao cha 56 cha baraza hilo.
Alisema miaka ya nyuma wanafunzi wa utabibu na
ualimu waliotaka kujiendeleza kimasomo, waliomba
moja kwa moja vyuoni hali ambayo ilisababisha
kuwapo kwa mgongano wa wanafunzi na huku baadhi
vikidahili wasio na sifa.
“Mfumo huo utatuwezesha siku ya mwisho ya kuomba
waweze kutoa majina waliochaguliwa ili kusiwe na
mwingiliano na zoezi hilo litafanywa na
Nacte…tumefungua maombi hadi Julai 31, mwaka
huu,” alifafanua.
Alisema udahili wa wanafunzi kwa ngazi ya
astashahada, stashahada na shahada, umeanza Baraza
limetoa usajili wa muda mfupi na mrefu kwa vyuo
mbalimbali 17.
Alisema usajili wa kudumu umetolewa kwenye vyuo
sita huku usajili wa wa miaka mitano kituo kina uwezo
wa kuendesha mafunzo.
Dk. Nkwera alisema usajili wa muda ambao ni wa
miaka miwili umetolewa kwa vyuo 11, huku Nacte
ikiandaa mitaala 17 itakayotumika kwenye vyuo
mbalimbali ili kuepuka kwa vyuo kuwa na mitaala
inayojirudia rudia na viwango vinavyotofautiania.
Alisema vyuo viwili vilipata usajili wa maandalizi,
haviruhusiwi kuchukua wanafunzi kwa sababu
havijafikia kiwango cha kutenda kazi.
“Kwa vyuo vya afya vilivyopewa usajili kabla ya kuanza
vinatakiwa kupata mitaala inayotolewa na Nacte na
kwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili
kujiendesha kwa vigezo na masharti ya uendeshaji wa
vyuo hivyo.
Vyuo 21 vyafutiwa usajili
Wakati huo huo, katibu huyo alisema vyuo 21
vimefutiwa usajili wake kwa kipindi cha miaka mitatu
kutokana na kushindwa kufikia vigezo vinavyotakiwa.
Kwa mujibu wa Dk. Nkwera, kuna jumla ya vyuo 372 na
kwamba vilivyofutiwa vilishindwa kujiendedsha kwa
mujibu wa sheria na taratibu.
Alisema vyuo vingi vilivyofutiwa vipo jijini Dar es
Saalam na vina msongamaono mkubwa wa wanafunzi,
kuanzisha kozi zisizo na kibali, kudahili wanafunzi
wasio na sifa na kutokuwa na majengo.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya Maendeleo ya Rasilimali
Watu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Otilia
Gowelle, alisema Mfuko wa Dunia na Taasisi ya
Benjamin Mkapa, watatoa udhamini kwa wanafunzi
1,401 na kiasi cha Shilingi bilioni mbili zimetengwa
kwa mwaka huu.
Alisema kwa mwaka huu wanatarajia kudahili
wanafunzi 6,255 na watakaopewa ufadhili ni wale
ambao wataingia mkataba wa kwenda kufanya kazi
kwenye maeneo ya vijijini yenye upungufu baada ya
kumaliza masomo yao.