SUAREZ ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA ENGLAND


image

Suarez na Hazard katika picha ya pamoja baada ya
kupokea Tuzo zao
Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool ‘Luis Suarez’
ameteuliwa kuwa mchezaji wa mwaka wa chama cha
wachezaji wa soka la kulipwa katika hafla iliyofanyika
jana jijini London.
Suarez alinyakuwa tuzo hiyo iliyotolewa na chama cha
wachezaji soka wanaolipwa kijulikanancho kama
Professional Footballers Association ‘PFA’ baada ya
timu anayochezea kufanya vizuri katika msimu huu
hapa akiwa amewabwaga wachezaji wenzake Steven
Gerrard pamoja na Daniel Sturridge.
Akiwa ametupia wavuni magoli 30 katika ligi kuu ya
England sambamba na hat -Trik mbili. Naye mchezaji
kinda wa Chelsea ‘Edzen Hazard’ ameteuliwa kuwa
mchezaji mdogo zaidi wa mwaka katika ligi kuu ya
England.