Ugomvi wa P- Square ilikuwa ni ‘Publicity stunt’? Muda mfupi baada ya ‘amani’ kurejea watangaza ujio wa album yao mpya!


Ugomvi uliowanyima raha mashabiki wa muziki wa
mapacha wa P-Square ilikuwa ni ‘publicity stunt’ ya
ujio wa album yao mpya?? Hilo ni swali ambalo sio
mimi pekee nimejiuliza, bali hata baadhi ya mashabiki
wa kundi hilo kutoka pande mbalimbali za Afrika
waliokuwa wakiliombea kundi hilo lisivunjike.

image

Paul Okoye wa P-Square kupitia ukurasa wake wa
Facebook jana ametangaza ujio wa album yao mpya
ikiwa ni muda mfu tu toka wathibitishe kuwa amani
imerejea Square ville..
“Wrapping that Album up!!! Get ready. Busy days ahead.
#ForeverPSQUARE” hiki ndicho alichokiandika Paul.
Hiyo ni habari iliyowafurahisha mashabiki wengi wa
kundi hilo, lakini hizi ni comments chache za baadhi ya
mashabiki wanaojua kuusoma mchezo:
– Nkiruka Alex Jayne -Publicity stunt or not I’m happy
that they sticking together but real talk the media are so
dramatic it’s very normal for siblings to fight and make
up lol
– Chidi L’chiny Ogbonna -I know that was why you guys
drew the attention of everybody with that so called fight.
– Chimelum Anizoba-Psquare ..so all those squables was
jst a publicity stunt..UNA TOO MUCH JARE..
– Bode Akinleye -#ForeverPSQUARE I know an album will
drop after the whole family drama LOL. Nice PR
strategy. Una too much
– Michael Ami Wasi-that publicity teaser was good,,we
called “communication”
Siku za mwanzo wakati ripoti za ugomvi wa mapacha
hao zinaanza kutoka, mtandao wa Naija Gists uliwahi
kumnukuu director mmoja wa Nigeria ambaye alidai
kuwa kwa uzoefu wake, alihisi kuwa kundi hilo
linakaribia kutoa album mpya hivyo aliamini hicho
kilichojitokeza ilikuwa ni ‘stunt’.
SOURCE: BONGO5