Filamu Aliyocheza Nicki Minaj Inaongoza Sasa Kwenye Filamu Kubwa Wiki Hii


image

Filamu iliyochezwa na mastaa wa Marekani “The Other
Woman” akiwemo rapper wa Young Money Nicki Minaj
imefika namba moja kwenye filamu kubwa wiki hii
kwenye American Box Office .
Filamu hii ya mapenzi na vituko yenye mastaa kama
Cameron Diaz, Leslie Mann,Kate Upton imefungua wiki
kwa kuingiza dola milioni 24.7 upande wa North
America, nakuishusha filamu ya Captain America: The
Winter Soldier.
Kwenye interview kuhusu husika wa Nicki Minaj kwenye
filamu hio Nicki alisema , “Nilikuwa najishtukia sana
sababu niko pembeni ya muigizaji kama Cameron Diaz
alafu nimesahau mistari ya kusema kwenye scene
yangu”
Filamu ya “The Other Woman”ilitegemewa kuingiza dola
milioni 17.

image

Hii sio filamu ya kwanza kucheza Nicki Minaj, sauti
yake ilisikika kwenye filamu ya Ice Age: Continental
Drift, iliyoingiza dola milioni 46 mwezi July 2012.