Baada ya adhabu ya boss mbaguzi, Diddy atainunua L.A Clippers?


image

Baada ya kuonekana uwezekano wa
timu ya L.A Clippers kuuzwa ili
mmiliki wa sasa asijihusishe nayo
tena baada ya kupewa adhabu ya
kutoisogelea maishani, P.Diddy
ameandika tweet ambayo kila mmoja
ameipokea kwa mtazamo wake.
Ameandika siku zote atakuwa
shabiki wa New York Knicks lakini
bado anabaki kuwa ni
mfanyabiashara na akamalizia na
hashtag ya DiddyBuyTheClippers.
Utajiri wake ni dola milioni 700 na
bado unaendelea kukua labda
ameshafikisha 800 hivi sasa au la na
Forbes wanasema L.A Clippers ina
thamani ya dola millioni 575 ambayo
ipo ndani ya uwezo wa Diddy lakini
itamgharimu zaidi ya nusu ya pesa
zake.

image