BEYONCE NDIYE MWANAMUZI MWEUSI ANAYEONGOZA KWA KULIPWA MKWANJA MREFU HIVI SASA


image

Beyonce Knowlesa ambaye ni mke wa Rapa Jay Z’,
ametajwa kuwa mwanamuziki wa kwanza mweusi
anayeongoza kulipwa mkwanja mrefu kuwahi kutokea,
huku akivunjilia mbali rekodi zilizowahi kuwekwa na
wakongwe kama vile Michael Jackson, Prince na Janet
Jackson baada ya mafanikio makubwa aliyoyapata
kupitia ziara yake ya muziki iliyopewa jina la ‘The
Mrs.Carter Show” World Tour .
Kwa mujibu wa jarida la Billiboard lilisema kwamba,
Beyonce ameweza kuingiza kiasi cha dola za
kimarekani milioni 212 katika kipindi cha mwaka
mzima alichokuwa akizunguka kufanya ziara zake za
kimuziki katika jumla ya miji 126 Duniani.

image

Awali hitmaker huyo wa Drunk in Love alifanya ziara ya
muziki katika bara la Ulaya iliyoanza mwezi Februari na
kumalizika mwezi machi ambapo alifanikiwa
kuzunguka katika miji ipatayo 25, na kumfanya aweke
kibindoni dola za kimarekani milioni 41.1 huku ngoma
kama vile Drunk in Love na XO zinazopatika kwenye
albamu yake ya tano ya Beyonce zikiendelea
kumpandisha chati kutokana na kupendwa zaidi na
mashabiki wake.
Tayari Beyonce ameshatangaza Ziara mpya ya muziki
iliyopewa jina la ‘On The Run’ atayofanya na mumewe
Rapa jay Z katika miji mikubwa 16 iliyopo Marekani na
Canada katika kipindi cha majira ya joto, itakayoanza
Juni 25 na kumalizika Agosti 05 mwaka huu katika
uwanja maarufu wa AT&T Park uliopo katika mji wa
San francisco.
Unaweza pia ukatazama hapo chini Tarehe pamoja na
orodha ya miji watakayopita katika ziara yao ya muziki
ya ‘On The Run’.
6/25 Miami, FL – Sun Life Stadium
6/28 Cincinnati, OH – Great American Ballpark
7/1 Foxborough, MA – Gillette Stadium
7/5 Philadelphia, PA – Citizen’s Bank Park
7/7 Baltimore, MD – M & T Bank Stadium
7/9 Toronto, ON – Rogers Centre 8
7/11 East Rutherford, NJ – MetLife Stadium
7/15 Atlanta, GA – Georgia Dome
7/18 Houston, TX – Minute Maid Park
7/20 New Orleans, LA – Mercedes-Benz Superdome
7/22 Dallas, TX – AT&T Stadium
7/24 Chicago, IL – Soldier Field
7/27 Winnipeg, MB – Investor Group Field
7/30 Seattle, WA – Safeco Field
8/2 Los Angeles, CA – Rose Bowl
8/5 San Francisco, CA – AT&T Park