Huyu ndiye msanii wa kwanza wa Bongo Fleva kupata Vevo Account.


image

Gosberth Kibanza aka Gosby msanii wa kizazi kipya
mwenye hit mbalimbali kama Monifere na Video yake ya
BMS ambayo ilivuka mipaka mpaka kituo cha channel O
ya Afrika Kusini amekuwa msanii wa kwanza wa kizazi
kipya kuwa accepted na VEVO na kumpa account ya
kuweka kazi zake za kimuziki.

image

VEVO ni mtandao wa internet unaoshughulika na video
za music na wanamuziki unaomilikiwa na kampuni
kubwa za muziki duniani SONY Music Group, Universal
Music Group, Warner Music Group na Google ,VEVO ni
mtandao number moja duniani unahusika na kuhifadhi
na kurusha kazi za muziki za wanamuziki maarafu
duniani, kama Jay Z, D’banj, Nick Minaj, Mafikizolo na
wengine wengi.
Msanii mwingine wa Tanzania ambae ana account ya
VEVO ni Rose Muhando ambae anafanya kazi na Sony
Afrika ambapo kuna stori kwamba ukiwa na account ya
VEVO kuna baadhi ya malipo unapata pale matangazo
yanapoonekana kwenye video yako.
Baada ya kupata Account hiyo ya VEVO Gosby
amesema >>’Nina furaha kubwa sana kwa kuwa mara
nyingi nimekuwa natamani kuwa na account ya VEVO,
VEVO ni platform kubwa ya wasanii na wadau wa
muziki duniani’
‘Nafurahi kuwa miongoni mwao sina shaka kazi zangu
zitatazamwa na wadau wakubwa wa soko la muziki
afrika na dunia,yah unaweza kuwa na video zako
youtube kama wanamuziki wengine au hata wasio
wanamuziki lakini VEVO ni maalum kwa Established
Musicians Only’
‘Hata mtu akitazama Music Video zako VEVO anakuwa
na uhakika kuwa hii ni video ya Established artist,
nadhani ni njia iliyosahihi kwa wanamuziki wa kizazi
kipya hapa nyumbani kujaribu kupata VEVO accounts’
‘Wenzetu wa Afrika Magharibi na Afrika Kusini
wanamuziki wao wote wakubwa wana VEVO accounts,
mapinduzi yetu ya muziki yasiishie kwenye platform za
hapa nyumbani tu, tutumie fursa zaidi za masoko na
kujitangaza kwenye mitandao mikubwa duniani’
‘Imeichukua management yangu takribani mwezi
mmoja na zaidi kufuatilia, kujaza form na mwishowe
kuwa accepted na VEVO inayopatikana kwenye
Youtube.com na VEVO.COM, nichukue fursa hii
kuipongeza management yangu kwa kazi nyingine bora
na yakujivunia na vile vile nitumie fursa hii
kuwapongeza mashabiki wangu kwa uvumilivu
waliokuwa nao katika kipindi hiki cha ku-migrate kazi
zangu kutoka youtube na kwenda VEVO ‘
‘video yangu ya BMS ilikuwa na Views 45,000 kipindi
tunaishusha ili kuweza kuhamia VEVO ikiwa ni moja ya
masharti ya VEVO ili kuzuia uzagaaji holela wa kazi”
Gosby pia ameongelea wimbo wake mpya anaotarajia
kuutoa hivi karibuni aliomshirikisha Ommy Dimpoz
>>’Yeah nina kazi nyingi ambazo ziko kwenye studio
tofautitofauti ambazo nimefanya na producers tofauti
tofauti kama 10 hivi na zimefanywa na producers
tofauti kama 7 wa hapa nchini na nje ya nchi’.
Source: TZA