NBA YAMFUNGIA MAISHA MMILIKI WA CLIPPERS ‘DONALD STERLING’ PAMOJA NA FAINI YA DOLA 2.5MIL


Shirikisho mpira wa kikapu nchini Marekani lijulikanalo
kama ‘NBA’ liimemfungia maisha mmiliki wa Timu ya
Los Angels Clippers Donald Sterling kufuatia agizo
lililotolewa na kamishina wa ligi hiyo ‘Adam Silver’
sambamba na faini ya dola za Marekani milioni 2.5
ikiwa ni pamoja na kutotakiwa kuhudhuria mechi za
timu hiyo, mazoezini au kufanya maamuzi yoyote ndani
ya timu hiyo .
Hiyo ni baada ya kukiri wazi mazungumzo baina yake
na kimada wake Stiviano kunaswa kwenye tepu rekoda
alipokuwa akimsisitizia kutopiga picha na watu weusi
ikiwemo na kutomleta rafiki yake yeyote kwenye mechi
za Clippers.
Matamshi hayo yalionekana kuwachukiza ama si
kuwakera mastaa wakubwa kama vile mchezaji kikapu
wa zamani Magic Johnson, Snoop Dogg, Jadakiss, Lil
Wayne, Lebron James na wengine kibao.
Wadau mbalimbali wenye mikwanja yao tayari
wameshaanza kujitokeza kutaka kuichukua Timu hiyo
jumla jumla huku ina la Magic Johnson likipendekezwa
zaidi kuinunua Timu hiyo.
Hata tovuti ya timu hiyo kwa sasa tokea ilipokuwa hapo
awali na kuwa ”We Are One LA C” halikadhalika na logo
ya timu hiyo iliyowekwa rangi nyeusi huku nyuma yake
ikiwa na Rangi nyeupe..e

image

Muonekano wa Tovuti ya Clippers
baadhi ya Marapa, wacheza kikapu na wadau
mbalimbali wameonyesha kufurahishwa na uamuzi
uliotolewa na NBA. Haya ni baadhi tu ya maoni yao
kuhusiana na sakata hilo.

image

image