Mwanasiasa maarufu akamatwa Ireland


image

Polisi huko Ireland Kazkazini wamemkamata
mwanasiasa mashuhuri wa chama cha Sinn Fein ,Gerry
Adams kwa kuhusishwa na mauaji yaliyotokea yapata
zaidi ya miaka 40 iliyopita.
Adams anahojiwa kuhusu mauaji ya Jean McConville
ambaye alitekwanyara na kundi la waasi la IRA mnamo
mwaka 1972 na kisha akapatikana amepigwa risasi na
kuuawa .
Kiongozi huyo amekanusha kuhusika kivyovyote vile
akisema kuwa alijipeleka binafsi kuzungumza na polisi
ilikujaribu kusuluhisha madai hayo yaliyomwandama
kwa miaka mingi mno .
Adams anakanusha kuhusika kwa vyovyote vile na
utekaji nyara wala mauaji yake bi McConville ambaye
alikuwa mama wa watoto kumi .
Adams anazuiliwa kutokana na kifo cha mjane huyo
aliyetekwa nyara na kundi la IRA mwaka wa 1972 .
Madai haya yanafwatia mahojiano mjini Belfast mwaka
wa 2001-2006 baina ya chuo kikuu cha Boston
Marekani na wakereketwa wa vita hivyo vilivyonuiwa
kuikomboa Ireland kutoka kwenye minyororo ya ukoloni.

image

Kiongozi wa Sinn Fein Gerry Adams amekamatwa
Mahojiano hayo yalifanywa kwa misingi kuwa
mahojiano hayo yangewekwa siri hadi baada ya vifo vya
wahusika wakuu,lakini baada ya kesi za kutaka
kutambulika wahusika na wahasiriwa waliotoweka
wakati wa vita hivyo
chuo hicho kililazimishwa kutoa sehemu ya mahojiano
kwa serikali ya Ireland.
Mmoja kati ya watu 16 waliosemekana kutoweka ni bi
McConville .
Mjane huyo alilaumiwa na IRA kuwa mpelelezi wa polisi
lakini baada ya ufafanuzi wa polisi yapata mwaka wa
1999, McConville ilibainika kuwa hakuwa.
Kundi hilo la IRA lilikiri kutekeleza mauaji yake bi
McConville mwaka wa 1999 lakini mwili wake
ulipatikana mwaka wa 2003 ukiwa umetupwa kwenye
ufukwe wa bahari.
IRA inashtumiwa kwa kampeini na mauaji yaliyotikisa
Ireland kaskazini kwa takriban miaka thelathini.

Advertisements