Clouds Media yapata leseni ya urushaji wa matangazo katika nchi za falme za kiarabu


Kampuni ya Clouds Media International leo imetangaza
kuwa imepewa leseni ya kurusha matangazo katika nchi
za umoja wa falme za kiarabu (UAE). Akielezea kuhusu
leseni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo
Bwana Joseph Kusaga, amesema sasa kituo cha Clouds
TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa
mataifa mbalimbali.

image

Joseph Kusaga
Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni
maarufu sana kwa vijana nchini Tanzania, hata hivyo
sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo kwenye
Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa
vipindi kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa lugha za
Kiingereza na Kifaransa.
Akieleza zaidi Kusaga amesema, “Leo ni siku ya
kihistoria na alama ya hatua moja katika mpango wetu
wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa
kupitia matangazo kwa njia ya mitandao.”
Clouds TV kimataifa haitotoa tu burudani, lakini pia
itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja
wa nchi za falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za
kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina
yao. Vituo vya televisheni katika Umoja wa falme za
kiarabu vipo vingi na vyenye ushindani mkubwa, lakini
Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi ya
kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika
chaneli yenye uwezo wa kuwahudumia zaidi ya
watazamaji takribani milioni 3.5 kutoka katika nchi za
Afrika. Kwa sasa hakuna kituo kinachotoa huduma hii
na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.
Clouds TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani,
tamthilia, maigizo, ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo
kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za Mashariki,
Magharibi na Kusini mwa bara la Afrika na itapatikana
kwa watazamaji walio katika Umoja wa falme za
kiarabu kupitia huduma ya IPTV inayotolewa na Etisalat
na Du.
Clouds TV kimataifa itarushwa kupitia mamlaka ya Abu
Dhabi ijulikanayo kama twofour54, ikiungana na vituo
kama FOX na CNN. Clouds TV kimataifa itaanza
kurusha matangazo ya majaribio katika wiki chache
zijazo kabla ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.

Advertisements