VIDEO MPYA YA SAUTI SOL ‘NISHIKE’ YAFUNGIWA KUCHEZWA KWENYE VITUO VYA TV NCHINI KENYA


image

Ikiwa ni siku mbili zimepita tangu
Video mpya ya kundi la Sauti Sol
inayoitwa ‘nishike’
kuachiwa ,mamlaka ya Kenya
imeifungia video hiyo kuonyeshwa
kwenye vituo vya televisheni nchini
humo kwa kile kilichodaiwa kuwa na
picha nyingi zisizokuwa na maadili.
Akifafanua suala hilo hapo jana
kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za
Mdundo, kiongozi kinara wa kundi
hilo aitwae ‘Bienaime’ alisema video
yao imefungiwa kutokana na
kuonyesha picha ambazo hazifai
kutazamwa na watu walio na umri
chini ya miaka 18.
Hata hivyo Bien aliwashukuru
mashabiki kwa mchango wao
mkubwa walioutoa wa kuitazama
video hiyo kwenye akaunti yao ya
Youtube iliyo na jumla ya video 17 na
kuifanya kuwa miongoni mwa video
zilizotazamwa zaidi katika kipindi
kifupi tangu iwekwe ikiwa tayari
imeshatazamwa na watu zaidi ya laki
moja.
Wakili wa bendi ya Sauti Sol
amepanga kufikisha mahakama
malalamiko ya wateja wake ili
kuweza kuachiwa huru kwa video
hiyo sambamba na kuendelea
kuonyeshwa katika vituo mbalimbali
vya televisheni.
Hii sio mara ya kwanza kwa video za
nchini Kenya kufungiwa, kwani hata
kundi la P-Unit liliwahi kukumbana
na adhabu hiyo kali kufuatia video ya
wimbo wao wa ‘You Guy(Dat Dendai)
kufungiwa licha ya kuchukua Tuzo ya
Channel O kama video bora ya Afrika
Mashariki

Advertisements