HIVI NDIVYO DIAMOND ALIVYOWASHUKURU MASHABIKI WALIOMUWEZESHA KUNYAKUA TUZO 7 ZA KTMA 2014


image

Daima mtu anayepewa chakula na baada ya kushiba
akasema asante huyo anachukuliwa kuwa ni
muungwana, hivyo ndivyo alivyofanya Rais wa serikali
ya watu wasafi Tanzania, Diamond Platnumz aliyeweka
Rekodi ya kuwa msanii pekee wa kwanza Tanzania
kuweza kunyakua Tuzo nyingi za Kilimanjaro Tanzania
Music Awards 2014 tangu kuanzishwa kwake yapata
miaka 14 iliyopita.
Ushindi huo wa kishindo umemfanya Diamond avunje
rekodi zilizowahi kuwekwa na kaka zake akiwemo
mwanamuziki 20 Percent na bendi ya mashujaa
waliopata Tuzo tano tano kila mmoja mnamo mwaka
2012 .
Akionyesha kuwa mwenye wimngi wa furaha, Diamond
aliandika kupitia ukurusa wake wa Facebook aliweza
kuwashukuru mashabiki wake walioweza kumpiga kura
na kuibuka kidedea katika Tuzo hizo.
”Hakika ilikuwa ni kazi ngumu sana lakini kwa uwezo
wa mwenyez mungu ametufanyia wepesi na hatimaye
kufanikisha… Nawashkuru sanasana Mashabiki zangu
wote kwakuwa nyie ndio mlionipa tuzo hizi kupitia kura
zenu… Family, uongozi wangu.. bila kuvisahau vyombo
vyote vya habari vilivyo fanya kazi zangu zisikike kila
kona”. aliandika Diamond..
Aliongezea ”Niwashkuru pia wasanii wenzangu,
kwakuwa naamini wote walifanya kazi nzuri na
ndiomaana wote tukawa pale ila kwakuwa mshindi ni
mmoja, ikatokea kuwa bahati yangu…Ahsanteni sana,
cha mwisho nnachoweza kusema tu ni kwamba (Tika!
Tika!) yaani (Saba saba) Nomination 7 Tunzo 7…!
tuhamieni MTV Awards tuilete Heshima nyumbani
sasa”.

Advertisements