MTOTO WA PETER WA PSQUARE AWAPA UJUMBE MZITO WANAMGAMBO WA BOKO HARAM


image

Wakati nchi ya Nigeria ikiwa kwenye
hali ya simanzi kufuatia kupotelewa
kwa wanafunzi 234 wa shule ya kike
ya bweni iliyopo eneo la Chibok
katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja.
Familia ya mwanamuziki ‘Peter
Okoye’ anayeunda kundi la Psquare
iliweza kumtumia mtoto wao wa
kiume ‘Cameroon Peter Okoye’
kuweza kufikisha ujumbe kwa watu
wanaowashikilia wanafunzi hao.
”My name is Cameroon Okoye, Please
bring back our girls, please!” alisema
mtoto huyo kwenye video fupi
iliyorekodiwa kwenye simu ya mama
yake mzazi ambaye ni mke halali wa
Peter aitwae Lola Omotayo na kisha
kushea na mashabiki kwenye
ukurasa wake wa instagram
Hadi sasa ni takribani wiki mbili
zimepita tangu kutekwa kwa watoto
hao kupatikana licha ya jitihada
zinazoendelea kufanywa na serikali
ya Nigeria ikishirikiana na jeshi lake.
Tukio hilo ambalo limegusa hisia za
watu wengi hasa wazazi na
wanaharakati wa haki za binadamu
hali iliyopelekea kuanzishwa kwa
kampeni maalum iliyopewa jina la
Bring Back Our Girl.