Profesa J na Jose Chameleon waingia studio kufanya wimbo mpya


Joseph Haule aka Profesa J na Jose Chameleone ni
marafiki wa siku nyingi. Chameleone aliwahi kutumia
beat ya wimbo wake ‘Nikusaidieje’ kurekodi wimbo
aliomshrikisha mdogo wake Weasel, Bomboclat. Na
sasa Jose hao wawili wamekutana kufanya wimbo wa
pamoja.

image

Proffesor Jay,Jose Chameleon ,Lamar na Villy wakiwa
studio
Kupitia Instagra, Profesa Jay ameandika: Ndani ya
Mwanalizombe Studio usiku sana,Professor Jay
Josechameleon @lamarfishcrab @producer villy,Shidaa
mpya inakuja!!! STAY TUNED, Dar East African HEAVY
WEIGHTS, Stay Tuned,mpaka waombe poooh !!!!”

image

Profesa J na Jose Chameleone katika Hotel ya Southern
Sun jijini Dar es Salaam hivi karibuni
Chameleone alikuwa nchini kuhudhuria tuzo za Kili
ambapo alishinda tuzo ya wimbo bora wa Afrika
Mashariki.
SOURCE: BONGO5.