VIDEO : KANYE WEST AMPA SHAVU LA KUMSIKILIZA SHABIKI ALIYEDAI ANAUWEZO WA KUCHANA ZAIDI YAKE


image

Kanye akimsikiliza shabiki aliyekuwa akiimba mbele
yake.
Rapa na Mmiliki wa lebo ya GOOD Music ‘Kanye West’
mwishoni mwa wiki aliamua kumpatia nafasi ya
kumsikiliza shabiki mmoja aliyeonekana kuwa msanii
asiye na jina wa miondoko ya kufokofoka, wakati
alipokuwa akirudi kwenye makazi yake aliyokuwa
amepanga ya Soho eneo la west Hoolwood, mjini Los
Angels, Marekani,
Akiwa ameongozana sambamba na mpenzi wake Kim
Kardashian, kijana mmoja aliwafuata kwa nyuma na
kudai kuwa yeye ni mkali na angependa adhihirishe
uwezo aliokuwa nao mbele ya rapa huyo na baada ya
kupewa nafasi, msanii huyo aliweza kuimba kwa
mtindo wa freestyle hali iliyomvutia kanye na kumfanya
asimame pembezoni mwa nyumba yake huku
akimsikiliza na baada ya jamaa huyo kumaliza, Kanye
alimwambia amefanya vizuri lakini kwa wakati huo
anahitaji kwenda kupumzika.
Mpaka hivi sasa bado haijaweza kufahamika hatma ya
shabiki huyo kama ataweza kulamba shavu la
kusainiwa kwenye lebo ya rapa huyo licha ya uwezo wa
hali ya juu aliounyesha pasipo kujali uwepo wa kamera
nyingi zilizokuwa zikimmulika kipindi anachana mbele
ya hitmaker huyo wa Bounce.
Unaweza ukatazama hapo chini Tukio zima lilivyokuwa,
sio mchezo kumfata mtu kama Kanye West ambaye ni
miongoni mwa marapa wa kubwa na wenye mkwanja
mrefu, lakini huyu jamaa aliweza ingawa hii sio mara
ya kwanza kwani hata mwanamuziki Big sean aliweza
kupata shavu la kujiunga na Good Music kwa staili
inayofana na hii

KAnye  West Lets Fan Rap For Him In SoHo! HD HQ: http://youtu.be/RZajcsSa0fs