#BRINGBACKOURGIRLS : MASTAA WA NIGERIA WAUNGANA NA WAANDAMANAJI KUISHINIKIZA SERIKALI KUWAREJESHA WANAFUNZI WA KIKE 234 WALIOTEKWA NA BOKO HARAM


Vilio vya wazazi bado vinaendelea
nchini Nigeria kufuatia tukio la
mabinti wapatao 200 waliokuwa
wakisoma katika shule moja ya
bweni iliyoko katika mji mkuu wa
Abuja, eneo la Chibok katika
kitongoji cha Borno kutekwa na watu
wanaodaiwa kuwa ni wanamgambo
wa kikundi cha Boko Haram .
Masupastaa wengi nchini humo
tayari wameshajiunga kwenye
kampeni iliyopewa jina la #
BringBackOurGirls inayohamasisha
kikundi hicho kuwaachia huru
wasichana hao waliowashikilia
wanaokadiriwa kufikia 234 wakiwa
salama, kwani kutofanya hivyo ni
ukiukwaji wa haki za binadamu
Mastaa kama vile Banky W, Waje,
Yemi Alade, Lami Phillips na msanii
wa filamu kutoka Nollywood Omoni
Oboli mnamo may 05 waliungana
pamoja na wakazi wengine katika
eneo la Allen Avenue na kutengeneza
kundi la wakazi waishio mjini Lagos
ambao wote kwa pamoja waliweza
kuandamana mpaka ikulu ya Lagos
iliyopo katika eneo la Alausa huku
wakiimba nyimbo na kuishinikiza
mamlaka husika ichukue hatua za
haraka ili kuweza kutatua kilio hicho
kinachoongelewa na vyombo
mbalimbali vya habari Duniani huku
kukiwepo na taarifa kuwa hata wiki
iliyopita mastaa wengine akiwemo
Waje na Seun Kuti nao pia
waliandamana

L

image

ami Phillips

image

Banky W, Yemi Alade, Waje pamoja
na waandamanaji wengine
wakielekea eneo ilipo ikulu ya Lagos

Advertisements