Mtanzania mwingine akamatwa Airport Nairobi akiwa na mzigo wa dawa za kulevya.


Mwanaume mmoja Mtanzania
amekamwata katika uwanja wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi
Kenya akiwa amebeba dawa za
kulevya akiwa njiani kuelekea
Antananarivo ambapo mzigo huo
ulitokea Tanga kisha ukapita
Mombasa na baadae kwa ndege
mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na
Heroin ambazo zote zina thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 24 za
Kitanzania na dawa hizo alikua
ameziingiza katika njia ya haja
kubwa.
Mkuu wa kitengo cha CID katika
uwanja huo Joseph Ngisa amesema
mshukiwa alikamatwa JKIA na
akawekwa kwenye chumba cha
uchunguzi na baadae akatoa tembe
za cocain na tembe za Heroin na
tayari ameshapelekwa Mahaka

image

mani.

Mwezi March mwaka huu
watanzania wanne walikamatwa
katika uwanja huohuo
walipopatikana na heroin yenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni
75 za Kitanzania na wote
walifikishwa mahakamani na kukiri
kosa.
Wanawake watatu na mwanaume
mmoja kila mmoja akishtakiwa
kando kwa kosa la kusafirisha dawa
za kulevya na walikua wameingia
Kenya kupitia Namanga na
walikamtwa wakiwa njiani kuelekea
Hong Kong.
Kuanzia March 2014 mpaka leo hii
May ni jumla ya Watanzania watano
wamekamatwa kwenye kiwanja cha
ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika
za kusafirisha dawa za kulevya
kwenda kwenye mataifa mengine.
Source: TZA