APPLE KUINUNUA KAMPUNI YA DR DRE ‘BEATS ELECTRONICS’ KWA DOLA BILIONI 3.2!


Dr. Dre yupo njiani kuwa rapper wa
kwanza BILLIONAIRE pale kampuni
ya Apple itakapoinunua kampuni
yake yake Beats Electronics.

image

Kwa mujibu wa TMZ, Apple inadaiwa
itainunua Beats kwa gharama ya $
3.2 BILLION. Dre na mwanzilishi wa
Interscope, Jimmy Iovine ndio
walioanzisha kampuni hiyo. Dre na
Jimmy walianzisha kampuni hiyo
mwaka 2008 kwa kutengeneza
headphone lakini sasa
wanatengeneza pia spika, vifaa vya
sauti vya kwenye magari na mtandao
wa kustream muziki.
Deal hiyo inaweza kukamilika wiki
ijayo na itakuwa deal kubwa zaidi ya
kampuni Apple. Dre alikamata nafasi
ya pili kwenye orodha ya Forbes ya
wasanii wa hip hop matajiri zaidi
akiwa na $550 million nyuma ya
Diddy mwenye $700 million.
SOURCE: BONGO5