LUPITA NYONG’O APIGA CHATA IKULU YA MAREKANI, AKUTANA USO KWA USO NA RAIS OBAMA NA MKEWE


image

Pichani wa kwanza kulia ni mama
mzazi wa Lupita Nyong’o, Rais wa
marekani Barack Obama, Lupita
Nyong’o na Michelle Obama.
Mshindi wa Tuzo ya Oscar, mwigizaji
mwenye asili ya Kenya ‘Lupita
Nyong’o’ ameweza kupata nafasi ya
kupiga stori mbili tatu kwa lugha ya
kiswahili na Rais wa Marekani
‘Barack Obama’ baada ya kupata
mualiko rasmi wa chakula cha jioni
kutoka katika ikulu ya Marekani
maarufu kama White House.
Lupita akiwa ameongozana na
mama yake mpendwa, waliweza
kukutana na Mr.prezidenti pamoja
na mkewe Bi.Michelle Obama huku
wawili hao wenye asili ya Kenya
wakiripotiwa kuzungumza Lugha ya
Kiswahili katika maongezi yao hayo.
Kwa hivi sasa Lupita ni balozi wa
vipodozi vya Lancome huku akitajwa
kuwa miongoni mwa mastaa daraja
la kwanza Dunia akiwa na utajiri
unaokadiriwa kufikia dola za
kimarekani milioni 43 ukichangiwa
zaidi na mauzo ya filamu
aliyochezwa ya 12 years a slave.

image

Hapa ni pale utani ulipochukua
wakati wake