MKE WA RAIS WA MAREKANI ‘MICHELLE OBAMA’ AUNGA MKONO KAMPENI YA #BRINGBACKOURGIRLS


Kampeni ya #bringBackOurGirls imeonekena kugusa
hisia za watu wengi hali iliyopelekea kuungwa mkono
na watu mbalimbali mashuhuri hasa wale wanaojua
uchungu wa mwana akiwemo mke wa Rais wa
Marekani Michelle Obama, pamoja na wanamuziki
kama vile LudaCris, J ohn Legend, Naomi Campbell,
Jamie Foxy, Drake, Justine TimberLake, Alicia Keys,
2Face na wengine kibao.
Kwa huzuni kabisa, mastaa waliotajwa hapo juu
waliweza kuweka ujumbe kwenye akaunti na kurasa
wanazomiliki za kwenye mitandao ya kijamii wakitaka
kuachiliwa huru kwa wanafunzi wa kike 234 wa shule
ya bweni ya Chibok ambao waliotekwa na
wanamgambo wa kundi la Boko Haram yapata wiki
mbili zilizopita katika jimbo la Borno nchini Nigeria .
”Our prayers are with the missing Nigerian girls and their
families. It’s time to #BringBackOurGirls.” aliandika
mke wa Rais wa sasa wa marekani Bi.Michelle Obama
kwenye ukurasa wake wa

Twitter .

image

Michelle Obama

image

Justin TimberLake
2Face Idibia
Mastaa mbalimbali wakiwa na mbango yaliyobeba
ujumbe mzito wa ”Real Men Don’t Buy Girls” ikiwa ni
katika kupinga kitendo kinachofanywa na Boko Haram
cha kuwashikilia wasichana hao na kutaka kuwauza
kwa watu wa mataifa mengine .

Advertisements