THAILAND YAMSHITAKI RASMI WAZIRI MKUU WAKE ‘YINGLUCK SHINAWATRA’ KWA TUHUMA ZA UFISADI


image

Yingluck Shinawatra
Tume ya kupambana na ufisadi
nchini Thailand imemshitaki rasmi
waziri mkuu aliyeondolewa
madarakani Yingluck Shinawatra
kwa madai ya kupuuza jukumu lake
katika usimamizi wa mpango
uliokosolewa vikali wa kutoa ruzuku
ya mchele.

Hatua hiyo imekuja baada ya
mahakama ya katiba kumuondoa
madarakani waziri mkuu huyo
ambaye anatuhumiwa kwa kuruhusu
mpango huo wa mchele uliokuwa
sera muhimu katika utawala wake
kuendelea licha ya kushauriwa
kwamba ulikuwa ukitumiwa vibaya
na kuzongwa na ufisadi.
Uamuzi huo unamaana kuwa
mwanamama YingLuck atakabiliwa
na kura ya kumng’oa madarakani
katika baraza la seneti ikiwa theluthi
tano ya kura zitaunga mkono uamuzi
wa kumtia hatiani na anaweza
kuzuiwa kushiriki katika masuala ya
siasa kwa miaka mitano.

Advertisements