MASHABIKI 15 WAFARIKI DUNIA KWENYE MECHI YA TP MAZEMBE NA AS VITA NCHINI CONGO


image

Polisi wakiwarushia mabomu ya
machozi mashabiki
Mashabiki 15 wa soka wamekufa
kwa kukanyagana baada ya polisi
kufyatua mabomu ya kutoa machozi
kwenye kundi la watu kwenye uwanja
wa soka wa Stempede uliopo katika

jiji la Kinshasa, jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi nchini
humo wamesema mashabiki
walipatwa na hasira jana jioni baada
ya timu yao ya AS Vita Club
kuchapwa kwa bao moja kwa sifuri
na klabu ya Tp Mazembe toka mji wa
Lubumbashi .

image

Majeruhi akipatiwa huduma ya
kwanza na kikosi cha msalaba
mwekundu
Kiongozi mmoja wa mjini huko
‘Emmanuel Akweti’ amesema askari
polisi wanne walibughudhiwa na
mashabiki na walipofyatua mabomu
ya machozi ndipo mashabiki hao
wakaanza kukimbia na kukanyagana
hali iliyopelekea kusababisha vifo.
Aliongezea kwa kusema kuwa watu
hao 15 wamekufa kwa kukosa hewa
na wengine zaidi ya 24
wamejeruhiwa katika tukio hilo.