DIAMOND AZIDI KUNG’ARA, ATAJWA KUWANIA TUZO ZA BET AWARDS 2014


image

Tangu aweke rekodi ya kuzoa tuzo 7
za KTMA pamoja na kuchaguliwa
kuwania Tuzo za KORA na zile za
MTV MAMA, mshika kipaza wa
Tanzania ‘Diamond Platnumz’
ameendelea kuipeperusha vyema
bendera ya Tanzania baada ya
kuchaguliwa kwa mara ya kwanza
kuwania Tuzo kubwa kabisa za watu
weusi
zinazofahmika kama BLack
Entertainment Awards maarufu kama
BET huku akiwa msanii pekee
anayetokea Afrika Mashariki.
Katika Tuzo hizo, Diamond anawania
kipengele cha ‘Best International Act’
akichuana vikali na wakali kama vile
‘Davido’ kutoka Nigeria, kundi la
Mafikizolo la Afrika Kusini, Sarkodie
wa Ghana, Tiwa Savage kutoka
Nigeria pamoja na Toofan wa Togo.
”KWA SASA SINA MENGI YA
KUSEMA,ILA NAMSHUKURU
MWENYEZI MUNGU KWA HATUA
HII,NA SIWEZI SAHAU
KUWASHUKURU MASHABIKI WANGU
KWA SUPPORT MNAYONIPA NA
KUNI MOTIVATE NIZIDI KUFANYA
VIZURI KILA SIKU,NINA IMANI MDA
SIYO MLEFU MZIKI WETU
UTASOMEKA KWENYE RAMANI
TUNAYOITAKA,NIWAKUMBUSHE
TU,HIZI NI NOMINEES HATUA ZA
UPIGAJI KURA ZIKIANZA
NITAWAJULISHA.USISAHAU TU
KUENDELEA KUNIPIGIA KURA TUZO
ZA MTV MAMA,PIA KORA KWA
KULIKE PAGE YAO NA KU COMENT
JINA LANGU.AHSANTENI.” aliandika
Diamond kwenye ukurasa wake wa
Facebook wenye wafuasi zaidi ya
Laki na nusu .
Kilele cha Tuzo za BET ni Jumapili ya
June 29 mwaka huu mjini Los Angels
Marekani . KWa pamoja Watanzania
tunaweza kumpigia kura kwa wingi
Diamond ili kumuwezesha kunyakua
Tuzo hizo zote kubwa anazowania
kwa hivi sasa…

Advertisements