AFISA WA UMOJA WA MATAIFA ALAANI MAUAJI KIDAL


Mkuu wa kikosi cha umoja mataifa cha
kulinda amani nchini Mali analaani vikali
mauaji ya maafisa sita wa serikali na raia
wawili jumapili yalivyofanywa na
waliojitenga katika mji uliozingirwa wa
Kidal.
Albert Koenders anakiita kitendo hicho
hakikubaliki hata kidogo na uhalifu wa
kinyama na
kusema wale wanaohusika
lazima walipe.Sababu halisi ya mauaji
hayo bado haijajulikana.
Mauaji yalitokea jumapili wakati waziri muu
wa mali Moussa Mara alipopeleka vikosi
huko Kidal ili kuukomboa mji huo kutoka
kwa waasi wa Tuareg ambao
wanawashikilia mateka wafanyakazi 30 wa
serikali. Bw.Mara anasema nchi hiyo iko
vitani na waasi.
Mapigano kati ya majeshi ya serikali na
waliojitenga mpaka sasa yamepelekea vifo
vya watu 36 katika pande zote mbili .
Source:
http://www.voaswahili.com