HAYA NDIO MAPYA KUHUSU NDEGE YA MALAYSIA ILIYOTOWEKA ANGANI


image

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia amesema
Shirika Kuu la Kijasusi la Marekani CIA
linaficha maelezo muhimu kuhusu hatima ya
ndege ya Malaysia iliyotoweka. Katika taarifa
aliyochapisha katika weblogu yake siku ya
Jumapili, Mahathir Mohammad amesema CIA na
shirika la utengenezaji ndege la Marekani,
Boeing, kwa pamoja zinaficha maelezo kuhusu
ndege iliyotoweka. Aidha amesema ni jambo la
kushangaza kuona vyombo vikubwa vya habari
duniani havifuatlii kwa kina kadhia ya ndege
hiyo ya Malaysia. Mahathir amesema yamkini
CIA iliongoza ndege hiyo kwa mbali na kuiweka
katika mfumo wa kujiendesha yenyewe kisha
ikatua eneo la siri na alama zake za Malaysian
Airlines kuondolewa. Ndege hiyo ya Shirika la
Ndege la Malaysia iliyotoweka tarehe 8 mwezi
wa Machi mwaka huu ikiwa na mamia ya abiria
ilipokuwa inaelekea Beijing, China kutoka Kuala
Lumpur Malaysia. Pamoja na kuwa nchi kadhaa
zinashirikiana katika juhudi za kuitafuta ndege
hiyo kwa kutumia teknolojia ya kisasa lakini
bado hakuna athari zozote za ndege hiyo ya
kisasa aina ya Boeing 777-200ER
iliyotengenezwa Marekani. Waziri Mkuu wa
Malaysia Najib Razak naye pia alinukuliwa
akisema ndege ya abiria ya nchi hiyo
iliyotoweka ilipotoshwa mkondo wake kwa
makusudi na kuendelea kuruka angani masaa
kadhaa hata baada ya kutoweka kwenye rada.
SOURCE: DJ SEK

Advertisements