Kumbukumbu ya miaka 18 toka kuzama kwa MV Bukoba


RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga,
iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv
Bukoba, inasema usiku wa kuamkia
siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria
kati ya 750 na 800 pamoja na
wafanyakazi 37.
Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa
hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa
wamefariki na kuzikwa katika
makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji
la
Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa
na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili
332 haikupatikana.
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali
inayosema haina dini, huongozana na
viongozi wa madhehebu ya dini na
waganga, kwenda eneo la ajali kufanya
kumbukumbu.
Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha
wa mv Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru,
(sasa marehemu), Mkaguzi wa
Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa;
aliyekuwa Meneja wa Bandari ya
Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa
Maneja wa Bandari ya Kemondo,
Prosper Lugumila.

image

Meli ya Mv Bukoba ikiwa inazama.
Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998,
ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka
2001. Miongoni mwa waendesha
mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer
Feleshi.Hukumu ya kesi ilitolewa na
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu,
Juxton Mlay (sasa mstaafu), Ijumaa, 29
Novemba 2002, majira ya saa sita
mchana.
Washitakiwa wote walishinda kesi,
kufuatia hukumu ya kurasa 118
iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji
Mlay kusema, mv Bukoba ilizama kwa
sababu haikuwa na uwiano wa majini
na siyo uzembe wa washitakiwa.
Serikali iliahidi kukata rufaa; lakini
hadi leo majaliwa ya rufaa hiyo
hayajulikani; na baadhi ya
washitakiwa wamefariki dunia bila
kujua hatma ya kesi hiyo wala stahili
zao.
Kwa kipindi kirefu, mv Bukoba ilikuwa
‘kaburi’ lenye kuelea katika Ziwa
Victoria. Ilikwishapigwa marufuku
kufanya safari kwa kuwa haikuwa na
viwango vya ubora wa kuwa majini.

image

Makaburi ya Igoma ambako wahanga wa Mv
Bukoba walikozikwa
Meli hii ilijengwa na kampuni ya
Kibelgiji; ikazinduliwa 27 Julai 1979.
Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa
thabiti na ilikosa uwiano.
SOURCE:JF