WANAFUNZI WA KENYA WAPIGANA NA POLISI KUPINGA ADA KUONGEZWA


image

Wanafunzi walitawanywa kwa kutumia gesi ya
kutoa machozi
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya wamezua
vurugu wakipinga mpango wa serikali kutaka
kuongeza karo katika vyuo vikuu vyote vya
umma.

image

image

Polisi walipambana na wanafunzi hao kwa

kutumia gesi ya kutoa machozi kutawanya
wanafunzi hao ambao walizua vurugu mjini na
kuwapora abiria huku wakiharibu magari ya
umma na yale ya abiria katika barabara kuu ya
Uhuru katikakati ya jiji la Nairobi.
Pia waliripotiwa kuvunja maduka na kuharibu
mali ya watu.
Wachuuzi walilazimika kuondoka mjini huku
polisi wakipambana na wanafunzi hao ambao
waliungana kutoka vyuo vikuu mbali mbali kote
nchini Kenya.
Awali maandamano yao yalikuwa salama ingawa
baadaye wanafunzi hao walioanza kuandamana
tangu saa nne asubuhi walianza kuzua rabsha
na kulazimisha polisi kutumia mabomu ya kutoa
machozi kuwatawanya.
Wanafunzi hao wanaandamana kupinga
mapendekezo ya serikali kuongeza karo ya vyo
vikuu , ingawa waziri wa elimu ya juu Profesa
Jacob Kaimenyi amesema kuwa serikali bado
haijatoa tamko rasmi ikiwa wanafunzi wa vyuo
vikuu watalazimika kuongeza karo.
Alisema kuwa ripoti kuwa karo itaongezwa sio
sawa na ni za kupotosha akisisitiza kuwa ikiwa
jambo kama hilo litafanyika litahitajika
kutangazwa na baraza la vyuo vikuu nchini
humo baada ya makubaliano kufikiwa.
Wanafunzi hao wanapinga mpango wa serikali
wakisema kuwa kuambatana na mfumuko wa
bei, karo yao haipaswi kuongezwa na kwamba
serikali inapaswa kushauriana nao kabla ya
kufikia hatua zozote za kuongeza karo.
Wanafunzi watano wameripotiwa kujeruhiwa
katika vurugu hizo
SOURCE:DJ SEK (LUSEKERO DAVID)