Album mpya ya Michael Jackson ‘Xscape’ yakamata namba 2 kwenye Billboard 200


image

Miaka mitano baada ya kifo chake, mfalme wa
pop amerejea kwenye chart kwa album yake,
Xscape.
Album hiyo yenye nyimbo nane imeuza kopi
157,000 na
kukamata nafasi ya 2 kwenye chart
ya Billboard 200, kwa mujibu wa Nielsen
SoundScan. Xscape, inajumuisha nyimbo
zilizotayarishwa na wapishi kama Timbaland,
Rodney Jerkins, na Stargate. Hiyo ni album yake
ya 10. Album yake ya mwaka 2010 Michael
ilikamata nafasi ya 3 kwa kuuza kopi 228,000.
Wimbo wa kwanza kwenye album hiyo ni “Love
Never Felt So Good” aliomshrikisha Justin
Timberlake.