BALOZI MPYA WA MAREKANI AJITAMBULISHA KWA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS


image

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya
wa Marekani nchini Tanzani, Mark
Childres, wakati alipofika Ofisini kwake
Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 9, 2014
kwa mazungumzo na utambulisho wa
balozi huyo.

image

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo
na Balozi mpya wa Marekani nchini
Tanzania, Mark Childres, wakati alipofika
Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na
utambulisho wa balozi huyo.
Ikulu, Dar es Salaam: 2014-06-09
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed
Gharib Bilal leo amekutana na Balozi
mpya wa Marekani, Mheshimiwa Balozi
Mark Childress ambaye amefika ofisini
kwa mheshimiwa Makamu wa Rais kwa
ajili ya kujitambulisha.
Balozi Childress alimueleza Mheshimiwa
Mkamu wa Rais kuwa, Tanzania ni nchi
yenye uhusiano maridhawa na Marekani
na kwamba katika kipindi chake kama
Balozi atahakikisha uhusiano huu mzuri
uliojengwa unadumishwa na kwamba, nchi
hizi mbili zinazidi kuwa na maeneo ya
kushirikiana hasa yanayolenga kuboresha
maisha ya watu na kuwapatia maendeleo.
Balozi Childress pia alisema kuwa
Tanzania imekuwa ikitumia kama mfano
kufuatia kuonesha mabadiliko ya haraka
katika miradi mbalimbali inayoendeshwa
hapa nchini kwa ushirikiano na watu wa
Marekani na akafafanua kuwa, kazi
iliyoko mbele ni kuhakikisha kuwa
Tanzania inapiga hatua zaidi na sio
kurudi nyuma.
“Mheshimiwa Makamu wa Rais, kila
nikipata fursa ya kukutana na wenzangu
tumekuwa tukizungumzia suala la
Tanzania kupiga hatua kwa haraka. Mna
mambo mengi yaliyofanyika na kazi
iliyopo ni kuendelea kupiga hatua pasipo
kurudi nyuma,” alisema.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu
wa Rais alimueleza Balozi Childress kuwa,
Tanzania ipo katika kipindi ambacho
kinaonesha mabadiliko makubwa ya
kiuchumi na kwamba kazi ya serikali ya
Tanzania ni kuhakikisha kuwa uchumi
unakuwa na unasaidia vizazi vya sasa na
vijavyo.
“Mtazamo wetu katika serikali ni kuwa
Tanzania itapiga hatua kubwa katika
miaka michache ijayo. Lengo letu ni
kutazama kuwa ukuaji wa uchumi hauwi
wa muda mfupi, tunatazama pia
maendeleo kwa vizazi vijavyo.
Kuhusu suala la utunzaji mazingira,
Balozi Childress alisifu hatua za
Mheshimiwa Makamu wa Rais hasa katika
kazi ya uhamasishaji upandaji miti na
akasema, utunzaji wa mazingira ni jambo
la muhimu ili kuifanya nchi yetu iweze
kuendelea na isikabiliane na matatizo
yanayotokana na mazingira kuharibiwa.
“Nakupongeza Mheshimiwa Makamu kwa
kazi yako ya uhamasishaji utunzaji wa
Mazingira. Usichoke kufanya hivyo maana
unasaidia dunia,” Balozi Childress
alisema.
Imetolewa na : Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam

Advertisements