Taliban yakiri shambulizi Pakistan


image

image

Pakistan Taliban yakiri kutekeleza mashambulizi
Karachi
Msemaji wa kundi la Pakistan Taliban
Shahidullah Shahid amenukuliwa akisema kuwa
walitekeleza shambulizi hilo ilikumkumbusha
rais wa Pakistan Nawaz Sharif kuwa bado wepo
nchini humu na kuwa kundi hilo litaendelea
kutafutia haki mamia ya watu wanaouawa bila
ya hatia yeyote katika mashambulizi
ya ndege
zisizo na ruban kwa misingi ya kuwasaka
wapiganaji wa wataliban.
Waziri katika jimbo la Sindh , Qaim Ali Shah
alisema kuwa wapiganaji hao walikuwa
wamejiandaa vilivyo kutokana na jinsi
walivyotekeleza mashambulizi hayo katika eneo la
wageni mashuhuri katika uwanja huo mkuu mjini
karachi wa Jinna.
Inaaminika kuwa 14 kati ya wale waliuawa ni
maafisa wa usalama huku duru zingine zikisema
kuwa hata wahudumu wa ndege mbalimbali
waliathiriwa katika mkasa huo.
Mali ya thamani kubwa iliharibika lakini hakuna
ndege iliyoharibiwa katika mashambulizi hayo.
Kuna hofu kuwa bado kuna mshambuliaji mmoja
au hata wawili ndani ya uwanja huo.
Hata hivyo, Maafisa wanasisitiza kuwa sivyo.

image

Taliban yadai kutekeleza shambulizi katika
uwanja wa Ndege wa Karachi
Kwa sasa serikali imesema kuwa imedhibiti
uwanja huo na kuwa sasa uko salama kwa usafiri
wa ndege.
Ufyatulianaji risasi na makabiliano baina ya
wapiganaji wa kundi la Pakistan Taliban na
maafisa wa usalama wa Pakistan uliripotiwa
kuanza upya muda mchache uliopita katika
uwanja mkubwa kabisa wa ndege wa Pakistan
ulioko Karachi.
Hii ni baada ya mashambulizi ya usiku kucha
yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi hilo la Taliban.
Takriban watu 19 waliuawa katika ufyatulianaji
huo wa risasi, wengi wao wakiwa maafisa wa
usalama wa uwanja wa ndege.
Maafisa wa usalama wa Pakistani wamesema
kuwa washambulizi wote 10 waliuawa mwishowe
na kuwa uvamizi huo ulikuwa umeisha.

image

Taliban yadai kutekeleza shambulizi katika
uwanja wa Ndege wa Karachi
Mwandishi wa BBC aliyeko Islamabad Shahzeb
Jillani anasema uvamivi huo ulikuwa wa kijarisi
na bila shaka wa kujitolea mhanga.
Huu ulikuwa uvamizi wa kijasiri katika uwanja
mkubwa kabisa wa ndege nchini humo.
Baada ya zaidi ya saa tano za mapigano makali
na ufyatulianaji risasi , mkuu wa usalama wa mji
wa Karachi alisema kuwa wavamizi hao walikuwa
wameshindwa.
Lakini kidogo baadaye, milio ya risasi na milipuko
ilisikika tena na kuzua taharuki.
Waokoaji walionekana wakirudi tena katika eneo
la mashambulizi hayo.
Vituo vya habari vilionyesha picha za moto na
moshi ukifuka tena kutoka kwenye paa ya uwanja
huo.

Advertisements