Usher Alivyomtetea Justin Bieber Kuhusu Kufanya Ubaguzi wa Rangi


image

Kwa muda wa wiki mbili zilizopita
mwimbaji JustinBieber aliwekwa kwenye
kaa la moto la mashambulizi ya maoni
ya watu mbalimbali waliomkosoa baada
ya kuvuja kwa video vinazomuonesha
akifanya utani wa
ubaguzi wa rangi.

image

Justin aliomba radhi baada ya video ya
kwanza kutoka lakini kabla ombi lake
halijafika mbali iliachiwa video nyingine
ya pili inayomuonesha akifanya vilevile
kwa kubadili maneno ya wimbo wake na
kutumia N-Word. Video zote alirekodi
akiwa mtoto mwenye umri wa mika 15.
Mzigo umekuwa mzito kwa Justin Bieber
kutokana na jinsi dunia inavyochukulia
kwa umakini masuala ya kibaguzi.
Usher Raymond ambaye alimgundua
msanii huyo kupitia YouTube, ameamua
kumsaidia na kuandika ujumbe kwenye
Instagram kumtetea kwa kuwa anajua
alikuwa mtoto mdogo.
“Mimi ni mtu ambaye nasapoti ukuaji na
naelewa bila hukumu. Ukuaji huo unakuja
kama matokeo ya maumivu na bidii
endelevu. Kama nilivyokuwa nikiangalia
magumu anayopitia Justin Bieber kama
kijana mdogo. Naweza kuwaambia kuwa
daima hakuchagua njia ya uwezekano
wake kuwa mkubwa zaidi. Lakini bila
utata wowote sio mbaguzi wa rangi.
Allivyokuwa miaka 5 iliyopita alikuwa ni
mtoto asiye na uelewa na busara
ambaye hakuelewa nguvu hasi na
kutojali utu vinavyotokana na kucheza na
mzaha wa kibaguzi. Jinsi alivyo sasa ni
kijana mdogo ambaye banakabiliwa na
fursa za kuwa bora zaidi, mfano kwa
mailioni ya watoto wanaomfuata ili
wasifanye kosa hilo.”