Kumekucha Brazil, Dimba kung’oa nanga


image

Michuano kuanza Brazil
Kombe la dunia Brazil 2014 linatarajiwa kungo’a
nanga baadaye leo jioni huku Brazil na Croatia
wakitoana kijasho mjini Sao Paolo.
Dimba hilo litakalodumu kwa
mwezi mmoja,
litashuhudia mataifa 32 yakimenyana kuwania
kombe hilo katika fainali itakayochezwa mjini Rio
tarehe 13 Julai.
Mechi ya ufunguzi itaanza baada ya sherehe ya
kufungua mechi hiyo mjini Sao Paulo. Ni mechi
ambayo itakuwa inatoa kipaombele kuonyesha
umuhimu wa kukuza vipaji, utu na kabumbu.
“wacheni niwambie kuwa wakati umewadia.
Tunaenda sote . Hili ni kombe letu la dunia, ”
alinukuliwa akisema kocha wa Brazil Luis Felipe
Scolari.
Mwaka jana zaidi ya watu milioni moja walishiriki
katika maandamano ya kupinga hatua ya serikali
kuandaa michezo hiyo kwa gharama ya juu
wakati wananchi wengi wakiishi kwa umasikini.
Serikali ya Brazil iko makini kuzuia kutokea tena
kwa ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa
maandamano hayo. Rais Dilma Rousseff
amesema kuwa hatakubali kamwe maandamano
yanayosababisha ghasia kuathiri kombe la dunia.
Maelfu ya polisi na wanajeshi watashika doria
nchini humo kuhakikisha kuwa mechi zinafanyika
bila vurufu.
England itacheza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya
Italy Jumamosi tarehe 14 , mechi ambayo
itapeperushwa moja kwa moja na BBC.
Timu hiyo pia itacheza dhidi ya Uruguay na Costa
Rica katika kundi D.
Wenyeji Brazil wataanza mechi leo wakipigiwa
upatu kushinda kombe la dunia kwa mara ya sita
wakati mabingwa watetezi Hispania nao
wanakilenga kushinda kombe hilo kwa mara ya
nne baada ya kushinda ubingwa wa Ulaya miaka
miwili iliyopita.

Advertisements