Uingereza yasisitiza Miraa ni haramu


image

Kenya imelalamika kuwa Miraa ni kitega uchumi
cha jamii ya watu wa Meru
Uingereza imesisitiza kuwa marufuku
iliyowekewa mmea wa Miraa itaanza
kutekelezwa tarehe 24 mwezi Juni. Hii inafuatia
bunge la nchi hiyo kupitisha uamuzi wa serikali
ya Uingereza kuorodhesha miraa katika kundi la
dawa za kulevya.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Uingereza
imesema kuwa uamuzi huo haulengi Kenya moja
kwa moja. Imeongeza kuwa Serikali ya Uingereza
imekuwa ikidhamiria kwa muda mrefu
kuchunguza kisheria hali ya mmea huo.
Mapema mwezi uliopita wabunge kutoka maeneo
ya Meru kunakokuzwa kwa wingi mmea huo
walikuwa wametishia kuwasilisha bungeni hoja ya
kuwahamisha waingereza wanaomiliki mashamba
katika maeneo hayo ikiwa Uingereza itapiga
marufuku mmea huo.
Wabunge hao walikuwa wamesema kuwa

wakulima wa mmea huo watapata hasara kubwa
kwa sababu walikuwa wakiutegemea kukuza
uchumi wa eneo hilo.

image

Miraa ni kitega uchumi kwa wakazi wa eneo la
Meru nchini Kenya
Na kwa sababu hiyo Uingereza imesema kuwa
inatambua matatizo yanayowakumbuka
wazalishaji lakini itaendelea kushirikina na serikali
ya Kenya kwa kufadhili miradi ya kukuza uchumi.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Uingereza ilichukua
uamuzi huo baada ya kushauriana na washiriki
wake.
Nchi nyingi zenye uwezo mkubwa wa kiuchumi
yaani G8 zikiwemo Canada na Marekani
zimeharamisha Miraa iliyotajwa kuwa miongoni
mwa dawa za kulevya.
Mswada wa kupiga marufuku mmea huo
unaotumia mno Uingereza ulijadiliwa bungeni
machi na kuidhinishwa na bunge la chini na lile la
juu baadaye hivyo kuwa sheria.

Advertisements