Uchunguzi juu ya Bomu Zanzibar


image

Polisi visiwani Zanzibar wamewataka watu
kuendelea kutoa ushirikiano ili kuweza kupata
taarifa sahihi za watu wanaodaiwa kuhusika na
shambulio la bomu lililotokea visiwani humo.
Taarifa za polisi Zanzibar zilizotolewa Afisa
mwandamizi wa
Mkadam Khamis zinaeleza kuwa
hadi sasa uchunguzi aina ya bomu lililotumika na
wahusika wa shambulio hilo.
Hivi sasa visiwani Zanzibar kuna mkutano
mkubwa wa waumini wa dini ya Kiislamu kutoka
katika nchi za Afrika mashariki hali ambayo inatia
shaka kwamba huenda ndiyo walengwa wa
shambulio hilo.
Katika miaka ya hivi karibuni Zanzibar
imekumbwa na mashambulio ya mabomu
yanayolenga viongozi wa dini, watalii na nyumba
za ibada.
Mwezi februari mwaka huu shambulio jingine la
bomu lilitokea katika kanisa la Anglican karibu na
eneo la stone town lakini hakukua na maafa.