Zanzibar;Bomu lamuua mtu mmoja


image

shambulizi la bomu
Mtu mmoja ameripotiwa kufariki huku wengine
kadhaa wakijeruhiwa katika shambulizi la bomu
kisiwani Zanzibar.
Baadhi ya waathiriwa walikuwa wanaondoka
katika msikiti mmoja ulioko katika mji mkuu
wa
Stone Town.
Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo
ambalo linajiri mkesha wa sherehe za kimataifa
za filamu katika kisiwa hicho.
Ni shambulizi la pili la bomu mwaka huu.
Mnamo mwezi February, mabomu mawili tofauti
ya kujitengezea yalilipuliwa nje ya kanisa
Anglikana mjini Stone Town pamoja na mkahawa
uliokuwa karibu na kanisa hilo.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi wa kidini katika
kisiwa hicho.

Advertisements