Malkia amtunza Angelina Jolie


image

Wachezaji sinema, Daniel Day-Lewis na Angelina
Jolie, wametukuzwa na Malkia Elizabeth wa
Uingereza katika orodha anayotoa kila mwaka
kuwatunza watu waliotoa mchango mkubwa kwa
jamii.
Daniel Day-Lewis atapewa cheo cha
Sir, na
Angelina Jolie atapewa cheo cha Dame kwa
kampeni yake ya kupambana na uhalifu wa
ubakaji wa wanawake katika maeneo ya vita,
pamoja na kazi zake nyengine kwa niaba ya
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
wakimbizi, UNHCR.
Na waandishi wawili wa BBC wamepata nishani
ya OBE:
Lyse Doucet, mwandishi mkuu wa BBC katika
maswala ya kimataifa, na Tin Htar Swe, mhariri
wa Idhaa ya BBC ya lugha ya Burma.
Stephen Sutton, kijana wa miaka 19 aliyekufa
karibuni kutokana na saratani, na wakati akiugua
aliongoza mchango wa karibu dola milioni 7
kugharimia utafiti dhidi ya ugonjwa huo,
ametunzwa MBE, (ambayo alipokea kabla ya
kufariki mwezi uliopita.)
Mtunzi wa riwaya, Hilary Mantel, aliyeandika
vitabu vilivyopata zawadi ya Booker, ‘Wolf Hall’
na ‘Bring up the Bodies’, piya amepewa hadhi ya
Dame.

Advertisements