Kenyatta maarufu kwa Twitter Afrika


image

ais Kenyatta amempiku Paul Kagame wa Rwanda
kwa idadi ya wafuasi kwenye Twitter
Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais
anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa
Twitter barani Afrika.
Kenyatta amempiku Rais wa Rwanda Paul Kagame
na mwenzake wa
Afrika Kusini Jacob Zuma.
Kenyatta ambaye amekuwa mamlakani tu kwa
mwaka mmoja, amejipatia wafuasi 456,209, yuko
mbele ya mwenzake wa Rwanda Paul Kagame
mwenye wafuasi 408,353 ambaye amekuwa
mamlakani tangu mwaka 2000, miaka sita kabla
hata ya Twitter kuanzishwa.
Rais wa Afrika Kusini anayesifika kwa kashfa mbali
mbali, Jacob Zuma ana wafuasi 325,896 akishikilia
nafasi ya tatu.
Hata hivyo swali ni je maerais hawa hutumia vipi
Twitter? Je wao huwa na mazungumzo ya moja
kwa moja na wafuasi wao?
Waziri mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi
‘@AmamaMbabazi,’ ndiye kiongozi mwenye
kuwasiliana zaidi na wafuasi wake duniani kwenye
Twitter huku akiwajibu maswali yao kwake.

image

408,353, idadi ya wafuasi wa Rais Kagame kwenye
Twitter
Asilimia tisini na tano ya mawasiliano yake kwenye
Twitter ni ‘@replies,’ ishara ya kuwajibu wafuasi
wake. Utafiti huu ni kwa mujibu wa utafiti wa
kimataifa kuhusu viongozi wanavyojishughulisha na
Twitter, wenye mada, Twiplomacy.
Waziri mkuu mpya wa India, Narendra Modi ana
wafuasi milioni 4,967,847 , na anaelekea kushinda
Ikulu ya white House ambayo ina wafuasi milioni
4,976,734 katika nafasi ya tano.
Zaidi ya asilimia 83 ya mataifa yote duniani yana
uwakilishi katika Twitter, na asilimia 68 ya viongozi
wana akaunti za twitter kwa mujibu wa utafiti wa
shirika la Burson-Marsteller, nchini Marekani.
Viongozi wanaofuatwa sana kwenye Tiwtter ni
pamoja na Barack Obama (@BarackObama) akiwa
na wafuasi milioni 43, Papa Francis (@Pontifex) ana
wafuasi milioni 14 akifuatiwa na Rais wa Indonesia
Susilo Bambang Yudhoyono (@SBYudhoyono)
akiwa na wafuasi milioni tano.

image

Jacob Zuma kama rais anashikilia nafasi ya tatu
kwa idadi kubwa ya wafuasi wa Twitter Afrika
Rais Barack Obama alikuwa kiongozi wa kwanza
kuanzisha akaunti ya Twitter mwaka 2007.
Kati ya serikali 643 zenye akaunti za Twitter
ambazo zilitathminiwa katika nchi 161, ni mataifa 32
pekee hasa yaliyo Afrika na Asia ya Pacific ambayo
hayana shughuli nyingi kwenye Twitter.
Utafiti huo pia ulifichua kuwa mawaziri wa mataifa
ya kigeni hutumia sana Twitter kutafuta ushirikiano
wa kidiplomasia.

Advertisements