Wanawake wa Boko Haram wakamatwa


image

image

Jeshi la Nigeria limewakamata wanawake wafuasi
wa Boko Haram
Jeshi nchini Nigeria linasema limewakamata
wanawake watatu ambao walikua wanawaandikisha
wafuasi wanawake kwa kundi la Boko Haram.
Inadaiwa wanawake hao waliwalenga wajane na
wasichana wadogo wakiwaahidi kuwachumbia kwa
wafuasi wa Boko Haram.
Mwaandishi wa BBC Will Ross akiwa Abuja
anasema inaelekea Boko Haram inajaribu
kuwashawishi wanawake washiriki vilivyo katika
mapambano yao.
Mwezi
uliopita mshambuliaji mwanamke wa kujitoa
mhanga alifariki alipojaribu kuishambulia kambo ya
kijeshi katika jimbo la Gombe – tukio la kwanza aina
hiyo nchini Nigeria.
Bomu hilo lililipuka alipokua akipekuliwa katika kituo
cha usalama . Mwanajeshi mmoja pia aliuwawa.

image

Baada ya kuwateka wanafunzi sasa imebainika
Boko Haram inawafuasi wa kike.
Wanawake pia ni miongoni mwa wale
waliokamatwa na kuzuiliwa katika miji ya Maiduguri
kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo Boko Haram
wanaungwa mkono kiasi .
Jeshi la Nigeria limesema wanawake watatu
iliowakamata walikuwa ni wa tawi la upelelezi.
Ilisemekana mmoja wao alikua ni mjane wa
mpiganaji wa Boko Haram.
Kundi hilo la wanaharakati wa Kiislamu bado
linawashikilia zaidi ya wasichana wa shule 200
iliowakamata mnamo mwezi wa Aprili katika mji wa
Chibok katika jimbo la Borno .
Boko Haram inadai wapiganaji wake na jamaa zao
waachiliwe kwa kubadilishana na
wasichana.Serikali imelikataa dai hilo. .