Wanakijiji wataka Bangi ihalalishwe TZ


image

Watu wa Makete hutumia mbegu za Marijuana
kukaangia chakula tangu zamani
Huku harakati za kutaka matumizi ya Bangi
kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali
mbali duniani, Tanzania haijaachwa nyuma.
Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa
Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka
serikali iweke sheria ambayo itaweza kuhalalisha
matumizi ya mmea huo.
Wanakijiji hao zamani walikuwa wakitumia mbegu
za mmea huo kukaanga na chakula lakini siku hizi
wanalazimika kuzitumia kwa usiri mkubwa
wakihofia kukamatwa na polisi.
Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete
Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika
wilaya hiyo hayajaanza leo, tangu zamani watu
kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi
kukaanga na
chakula.
Na kama mmea huo ungekuwa na tahri kubwa
kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa
vichaa.

image

Majimbo mengi nchini Marekani yemahalalisha
utumiaji wa Marijuana kwa sababu za
kujistarehesha
Miti ya mimea hiyo pia ilikuwa ikitumiwa kutengeza
kamba ambazo anasema zilikuwa za nguvu sana.
Lakini kwa sababu ya sheria kali, matumizi ya
Bangi au Marijuana yanafanywa kichinichini katika
wilaya hiyo. SOURCE:
Mwandishi wa BBC Leonard Mubali