SEMINA YA FULSA YA UWEKEZAJI “DOING BUSINESS IN TANZANIA” YAFANYIKA LANDOVER, MARYLAND NCHINI MAREKANI


Kushoto ni Dkt. Frank Forka ambaye ni mkurugenzi PGCEDC Africa Trade Office akielezea njia za kufuata kwa mwekezaji kutoka Tanzania anapokuja kutafuta au kufanya mazungumuzo na wawekezaji wa Kimarekani kwa ajili ya kuingia nao ubia kwa ajili ya kuwekeza Tanzania. Dkt. Frank Furka alisema jambo la kwanza muhimu ni kujifunza utamaduni wa wafanyabishara wa Kimarekani hasa inapokuja kwenye swala la muda, Mambo mengine ya kuzingatia ni ufafanuzi wa kina na uwazi wa fulsa unayoitafutia mwekezaji na itakapokuja swali uwe na uwezo wa kulijibu kwa ufasaha.

Caroline Chang kutoka Maryland Center For Foreign Investment akielezea sheria ya EB-5 Invester’s Program inavyoweza kumnufaisha mwekezaji kutoka Tanzania anayewekeza nchini Marekani.

Jessca Mushala Mkurugenzi wa SHINA akielezea wawekezaji kutoka Tanzania wanahitaji mafunzo kwanza jinsi ya kujieleza, kuandika poropozo na kujifunza utamaduni wa wafanyabishara wa Kimarekani kabla hajakuja nchini Marekani. Jessca Mushala aliongezea kwamba anampango wa kumtuma mmoja ya mwakilishi wa SHINA kwenda Tanzania kufanya semina na wawekezaji wa Tanzania na kuwapa mafunzo ya nini cha kufanya wanapokuja Marekani kutafuta wawekezaji wanaotaka kuingia nao ubia.

Kutoka kushoto ni Mzee Zuberi, Stanslaus Munyaraga Malima na Awadhi Zuberi Athman wa kampuni ya Urban and Rural Engineering Services Ltd. Awadhi na Malima wapo nchini Marekani wakijaribu kujinadi kwa wawekezaji wa Kimarekani watakaoingia nao ubia kwenye fulsa ya uwekezaji ya umeme wa jua ikiwemo vifaa vya ujenzi.

Kulia kwa Jessca Mushala ni Mujuni Joseph Kataraia akielezea kampuni ya Urban and Rural Engineering Services Ltd na aina gani ya mwekezaji wanaemtafuta kuingia nae ubia wa uwekezaji wa umeme wa jua na vifaa vya ujenzi.

Dr..Loleta Robinson anayejihusiha na bishara ya vifaa vya hospitali na maabara akielezea uzowefu wake na Tanzania na kuchangia utamaduni wa swala la muda akijitolea mfano yeye mwenyewe alipokua Tanzania iibidi ajifunze utamaduni wao muda. Tanzania ukitaka kufanikiwa kilichokupeleka inakubidi uvumilie swala la muda kwani kuchelewa kwenye vikao ni jambo la kawaida. Dr. Loleta aliongezea alisema baada ya kufahamu hilo alichokua akifanya ni kuwahi huku akiwa na kitabu chake alichokua akikisoma huku akiendelea kuwasubili wahusika. Kulia ni Shaban Mseba aliyekuja kwenye semina hiyo kutoka New York.

wawakilishi kutoka SHINA wakifuatilia semina

Picha ya pamoja

Picha ya pamoja.

Kwa hisani ya Vijimamambo.

Advertisements