Baada ya adhabu ya boss mbaguzi, Diddy atainunua L.A Clippers?


image

Baada ya kuonekana uwezekano wa
timu ya L.A Clippers kuuzwa ili
mmiliki wa sasa asijihusishe nayo
tena baada ya kupewa adhabu ya
kutoisogelea maishani, P.Diddy
ameandika tweet ambayo kila mmoja
ameipokea kwa mtazamo wake.
Ameandika siku zote atakuwa
shabiki wa New York Knicks lakini
bado anabaki kuwa ni
mfanyabiashara na akamalizia na
hashtag ya DiddyBuyTheClippers.
Utajiri wake ni dola milioni 700 na
bado unaendelea kukua labda
ameshafikisha 800 hivi sasa au la na
Forbes wanasema L.A Clippers ina
thamani ya dola millioni 575 ambayo
ipo ndani ya uwezo wa Diddy lakini
itamgharimu zaidi ya nusu ya pesa
zake.

image

JE, DAVIDO ANA HARAKATI ZA KUPIGA COLLABO NA WALE WA MAYBACH ?


Rapa kinda wa Nigeria anayekuja
kwa kasi kama treni ya umeme, hapa
namzungumzia Davido, ameonekana
akiwa kwenye studio za Rapa wa
marekani mwenye asili ya Nigeria
‘Wale’ anayefanya kazi chini ya lebo
ya Maybach Music Group
inayomilikiwa na Rick Ross .
Wakiwa studio, mastaa hao waliweza
kupiga pamoja picha na kisha
kuzitupia mtandaoni. “Chilling at my
spot wit @lifeofdavido writin these
naija tunes” aliandika Wale kupitia
ukurasa wake wa Instagram.
Bado haijaweza kufahamika kama
wawili hao wapo kwenye mchakato
wa kufanya nyimbo pamoja au la,
licha ya dalili kujionyesha. Endelea
kutembelea blog hii kuhusiana na
taarifa zaidi.

image

image